Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

04 JANUARI 2021

Katika Jarida la Habari za umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea

-Watu zaidi ya 100 wauawa katika shambulio kwenye jimbo la Tillaberi nchini Niger, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani vikali shambulio hilo na kutaka wahusika wakamatwe na kuwajibishwa.

-Nchini Pakistan wachimba migodi ya makaa ya mawe 11 wameuawa katika shambulio la kigaidi lililotokea mwishoni mwa wiki kwenye jimbo la Balouchistan, watu wengine wengi wamejerihiwa na wengine kutekwa .

Sauti
10'6"
UN News

Tuna njaa, ni maafa, asema mkimbizi wa Syria aliyeko Lebanon. UNHCR inajitahidi kusaidia. 

Ripoti hiyo ya Benki ya Dunia na UNHCR imechunguza madhara ya ugonjwa wa COVID-19 katika kuwasukuma wakimbizi wa Syria katika umaskini, wao pamoja na wenyeji wao nchini Jordan, Lebaon na aneo la Kurd nchini Iraq.  Ahimidiwe Olotu na taarifa zaidi.

Ripoti hiyo inasema watu wanaokadiriwa kufikia milioni 4.4 katika jamii wenyeji, na pia takribani wakimbizi milioni moja wa Syria, na Wairaq wengine 180,000 waliokimbia makazi yao wameanguka chini ya mstari wa umaskini tangu mwanzo wa janga la COVID-19. 

Sauti
2'36"
Wakimbizi nchini Mauritani wamerejea shule baada ya kufunguliwa baada ya miezi kadhaa kufuatia kuzuka kwa COVID-19.
© UNICEF/Raphael Pouget

COVID-19 inaongezeka Afrika, hatua thabiti zinahitajika-WHO

Maambuki ya COVID-19 katika ukanda wa Afrika yameongezeka kwa kasi katika miezi miwili iliyopita, hali hiyo ikisisitiza hitaji la hatua za afya za umma zilizoimarishwa ili kuzuia kuongezeka kwa maambukizi, hasa wakati watu wanapokusanyika au kusafiri kwa sherehe za mwisho wa mwaka, imeeleza taarifa ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, iliyotolewa hii leo mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo.

Msichana kutoka Kenya akisomea nyumbani wakati wa vikwazo kukabiliana na janga la COVID-19.
© UNICEF/Brian Otieno

UNICEF yahimiza serikali duniani kufungua shule, japo kwa tahadhari

Idadi ya watoto wa shule walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 imeongezeka kwa asilimia 38 mwezi uliopita wa  Novemba, hali hiyo ikiweka mkwamo mkubwa kwenye maendeleo ya masomo na ustawi wa wanafunzi zaidi ya milioni 90 ulimwenguni, limeeleza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

Sauti
2'57"