Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Mwanamke akipimwa Covid-19 katika kliniki huko Palestina
©UNDP/Abed Zagout

Omicron isidharauliwe na kukosa usawa wa chanjo kunatuumiza zaidi - WHO

“Kutokana na kuenea kwa mnyumbuliko mpya wa omicron katika maeneo yote duniani, maambukizi mapya yalifikia milioni 9.5 na vifo vilizidi 41,000 ulimwenguni kuanzia Desemba 27 hadi Januari 2. "Na tunajua kwamba namba hizi ziko chini ya zile halisi." Anaonya Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt Tedros Ghebreyesus akitoa wito kwa mara nyingine tena kwa usambazaji sawa wa chanjo dhidi ya virusi vya corona.