Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yapendekeza dawa mbili mpya za kutibu wagonjwa wa COVID-19

Kinga mwili ya Sotrovimab ya sindano ni moja ya dawa mbili zilizopendekezwa na WHO kutibu wagonjwa wa Covid-19. Nyingine ni ya kumeza ambayo ni Baricitinib
© GlaxoSmithKline
Kinga mwili ya Sotrovimab ya sindano ni moja ya dawa mbili zilizopendekezwa na WHO kutibu wagonjwa wa Covid-19. Nyingine ni ya kumeza ambayo ni Baricitinib

WHO yapendekeza dawa mbili mpya za kutibu wagonjwa wa COVID-19

Afya

Kundi la wataalamu wa miongozo wa WHO wametaja dawa ya Baricitinib kwa ajili ya kutibu wagonjwa mahututi  wa COVID-19.Dawa nyingine iliyopendekezwa na wataalamu hao ni Monoclonal, na pia kutoa masharti ya matumizi ya kingamwili hiyo kutumika kwa wagonjwa walio na Covid-19 isiyo kali, lakini tu kwa wale walio katika hatari kubwa ya kulazwa hospitalini.

Wataalamu hao wa WHO wamesema mapendekezo ya leo yanatokana na ushahidi mpya kutoka kwa majaribio saba yanayohusisha zaidi ya wagonjwa 4,000 walio na maambukizi ya COVID-19 yasiyo makali, makali na makali zaidi.

Kundi hilo la wataalamu limesema mapendekezo yao yametokana na  ushahidi kwamba inaboresha maisha na inapunguza mahitaji ya kuwekewa hewa ya oksijeni kusaidia kupumua bila kuongezeka kwa athari mbaya.

Dawa nyingine iliyopekezwa na wataalamu hao ni Monoclonal na pia kutoa masharti matumizi ya kingamwili hiyo kutumika kwa wagonjwa walio na covid-19 isiyo kali, lakini tu kwa wale walio katika hatari kubwa ya kulazwa hospitalini.

Pamoja na mapendekezo hayo wamekiri kuwa mpaka sasa hakuna takwimu za kutosha kupendekeza matibabu ya kingamwili moja dhidi ya nyingine na wanakubali kwamba ufanisi wao dhidi ya aina mpya za virusi vya COVID-19 kama vile Omicron bado hauna uhakika na kwamba mapendekezo ya matumizi ya kingamwili yatakuwa yanaendelea kuboreshwa.

Wataalamu hao wa WHO wamesema mapendekezo ya leo yanatokana na ushahidi mpya kutoka kwa majaribio saba yanayohusisha zaidi ya wagonjwa 4,000 walio na maambukizo ya COVID-19 yasiyo makali, makali na makali zaidi.

Wamesema mara zote mapendekezo yao yanategemea ushahidi wa uhakika wa wastani kwamba inaboresha maisha na inapunguza haja ya kuwekewa hewa ya oksijeni kwa ajili ya kusaidia upumuaji na bila kuongezeka kwa athari mbaya.