Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Kinga mwili ya Sotrovimab ya sindano ni moja ya dawa mbili zilizopendekezwa na WHO kutibu wagonjwa wa Covid-19. Nyingine ni ya kumeza ambayo ni Baricitinib
© GlaxoSmithKline

WHO yapendekeza dawa mbili mpya za kutibu wagonjwa wa COVID-19

Kundi la wataalamu wa miongozo wa WHO wametaja dawa ya Baricitinib kwa ajili ya kutibu wagonjwa mahututi  wa COVID-19.Dawa nyingine iliyopendekezwa na wataalamu hao ni Monoclonal, na pia kutoa masharti ya matumizi ya kingamwili hiyo kutumika kwa wagonjwa walio na Covid-19 isiyo kali, lakini tu kwa wale walio katika hatari kubwa ya kulazwa hospitalini.