Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 JANUARI 2022

13 JANUARI 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo katika habari za Umoja wa Mataifa


Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema kuwa japokuwa habari mbayá ni kuwa Omicron ambao ni mnyumbuliko wa virusi vya corona ulichochea wimbi la nne la Covid-19 barani Afrika lakini unapungua haraka kuliko mawimbi yaliyotangulia kama lile la mnyumbuliko aina ya Delta. Hata hivyo idadi ya waliopata chanjo dhidi ya Covid-19 barani humo baado ni ndogo mno.  


Taasisi ijulikanayo kwa jina na Marafiki wa akina mama au Friends of Mothers iliyoko Mbale nchini Uganda imefanikiwa kuinua maisha ya zaidi ya familia 200 kutoka vijiji 7 baada ya kuwapatia ajira kwenye sekta ya kilimo.


Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA baada ya kuona athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, moja ya mbinu za kuleta suluhu kupitia kukuza kipato miongoni mwa wakulima wa eneo la Timbuktu, wameibuka na mradi wa kuboresha bustani yao ya soko la mboga na sasa nuru ya kujipatia kipato imeonekana.
 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'31"