Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/ Assumpta Massoi

Simulizi: Jina langu ni Selemani lakini nilikuwa naitwa Selina

Wakati kila kona ya dunia kwa sasa ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, harakati hizo miaka ya 1987 hazikuwa rahisi kueleweka ndani ya baadhi ya jamii kwani mila na destuli ambazo nyingine zilijikita katika mfumo dume ndizo zilizokuwa zimetamalaki. Lakini wanaharakati walitumia mbinu mbalimbali hata kubadili majina ili waweze kufanya kazi ya kubadilisha mitazamo ndani ya jamii.

Sauti
3'18"
UN News/ Byobe Malenga.

Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC

Hivi karibuni tulinukuu mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF yakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kushamiri hivi karibuni kwa mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mapigano makali kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami katika muda wa wiki sita tu yamesababisha watu 450,000 kukimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Sauti
3'19"
© UNICEF/Zahara Abdul

Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF

Kwa mujibu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF), tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe kwasababu zinachangia kuongezeka uzito usio salama kiafya, na vyakula hivyo vinaweza kuchukua nafasi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa watoto.

Sauti
3'37"
© UNICEF/Paul Kidero

Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama

Wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini.

Sauti
4'33"
UN News/Daniel Dickinson

Juhudi za pamoja zimesaidia kudhibiti kipindupindu Zanzibar: WHO

Mtazamo wa kujumuisha sekta mbalimbali na kuishirikisha kikamilifu jamii imekuwa chachu kubwa ya kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu iliyokuwa ikikiandama kisiwa cha Zanzibar kwa muda mrefu limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Mtazamo huo ambao unaunganisha kampeni za uelimishaji kwa jamii kupitia ufadhili wa muungano wa chanjo duniani GAVI na msaada wa wadau mbalimbali likiwemo shirika la WHO imekisaidia kisiwa hicho kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa kipindupindu katika miaka mitano iliyopita. Ungana na Flora Nducha kwa makala hii kwa kina.

Sauti
3'45"
UNICEF/Frank Dejongh

Tiko: Jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi launganisha vijana Kenya

Umoja wa Mataifa nchini Kenya, kupitia ushirikiano unaoongozwa na UNFPA, UNAIDS, WHO, na Jukwaa la Ushirikiano wa SDG, chini ya uratibu wa jumla wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Serikali ya Kenya, shirika la kimataifa la Triggerise, Children's Investment Fund Foundation (CIFF), and Bridges Outcomes Partnerships wanatekeleza mradi wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya kupitia huduma ya Tiko ya shirika la Triggerise. Kiujumla huduma ya TIKO inalenga kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15 - 19

Sauti
4'4"
UNICEF/Eyad El Baba

Huduma za afya Al-Shifa zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali - WHO

Tangu October 7,2023 mzozo unaoendelea nchini Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas umesababisha idadi kubwa ya vifo na majeraha kwa raia na wafanyakazi zaidi ya 100 wa Umoja wa Mataifa. katika ukanda wa Gaza mashambulizi ya anga na ukosefu wa vifaa vya matibabu, chakula, maji na mafuta vimeathiri mfumo wa huduma za afya ambao tayari unakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali.

Sauti
3'39"
WFP Video

Gaza hali ni tete lazima misaada zaidi ipelekwe: WFP

Hali kwa raia walioko Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá kila uchao hasa kutokana na kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel za agani na ardhini zilizosababisha maelfu ya raia kuendelea kutaabika kwa kukosa mahitaji muhimu ya msingi kama chakula, maji, huduma za afya na mawasiliano limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.

Sauti
4'10"
UN News/Assumpta Massoi

Vijana tusiwe watazamaji bali tuchukue hatua kwa kuanza na tulicho nacho- Emmanuel

Vijana wana dhima kubwa katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo mwaka 2030. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi hiyo ya vijana wanatumia vijana wenyewe ili wawe mabalozi wa mashirika hayo mashinani ili kupigia chepuo yale yaliyomo kwenye SDGs. Mathalani nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina mabalozi na miongoni mwao ni Emmanuel Cosmas Msoka yeye akijikita kwenye masuala ya usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu.

Sauti
3'33"