Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama

Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama

Pakua

Wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya kuhusu changamoto za choo katika eneo hilo unangana naye..

Audio Credit
Leah Mushi/Pamela Awuori
Audio Duration
4'33"
Photo Credit
© UNICEF/Paul Kidero