Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tiko: Jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi launganisha vijana Kenya

Tiko: Jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi launganisha vijana Kenya

Pakua

Umoja wa Mataifa nchini Kenya, kupitia ushirikiano unaoongozwa na UNFPA, UNAIDS, WHO, na Jukwaa la Ushirikiano wa SDG, chini ya uratibu wa jumla wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Serikali ya Kenya, shirika la kimataifa la Triggerise, Children's Investment Fund Foundation (CIFF), and Bridges Outcomes Partnerships wanatekeleza mradi wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya kupitia huduma ya Tiko ya shirika la Triggerise. Kiujumla huduma ya TIKO inalenga kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15 - 19

Tiko ni jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi ambalo huunganisha vijana waliobalehe kwenye vituo vya karibu vya umma na vya kibinafsi vinavyotoa huduma bila malipo. Mfumo wa Tiko unawaleta pamoja wahusika wakiwemo mitandao ya kliniki za afya, maduka ya dawa, mitandaoni, mashirika ya kijamii, na wahudumu wa afya wanaosaidia vijana katika kufanya uamuzi wao kwa huduma za afya na ustawi wanazohitaji ili kustawi. Kupitia mfumo wa kidijitali, Triggerise inaweza kufuatilia kila senti inakoenda na kutathmini matokeo yake kila siku kwa ripoti za wakati halisi na maarifa yanayotokana na takwimu.

Audio Credit
Anold Kayanda/Evarist Mapesa
Audio Duration
4'4"
Photo Credit
UNICEF/Frank Dejongh