Mfumo wa AFCAFIM unaoratibiwa na IFAD wawezesha wakulima Kenya kuhimili mabadiliko ya tabianchi
Kwa miaka 45, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo , IFAD umekuwa ukifadhili wakulima wadogo wadogo na maendeleo vijijini. IFAD inakuwa kama mratibu kwa kushirikiana na benki binafsi na sasa kuna mfumo wa fedha wa kuwezesha wakulima Afrika kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi au ARCAFIM. Mfumo huo umewezesha kupatikana kwa dola milioni 700 za uwekezaji kutoka sekta binafsi kwenye kwa wakulima wadogo huko Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda, ili kutokomeza umaskini na njaa katika maeneo ya vijijini ya nchi zinazoendelea.