Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF

Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF

Pakua

Kwa mujibu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF), tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe kwasababu zinachangia kuongezeka uzito usio salama kiafya, na vyakula hivyo vinaweza kuchukua nafasi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa watoto. Matumizi ya vyakula na vinywaji vitamu kwa watoto wachanga na watoto wadogo huongeza uwezekano wa kuharibika kwa meno na tatizo la kiribatumbo kwa watoto.  Kiujumla matumizi ya vyakula visivyo salama kiafya inamaanisha vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi na mafuta yasiyo salama kiafya. 

Edisoni Tumaini Anatory wa redio washirika wetu Karagwe FM ya wilayani Karagwe, mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania ametuandalia makala hii akiangazia mamlaka za afya kwa umma katika hiyo zinavyotoa wito kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususani kwa watoto wadogo.

Audio Credit
Anold Kayanda/Tumaini Anatory
Audio Duration
3'37"
Photo Credit
© UNICEF/Zahara Abdul