Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/Assumpta Massoi

Mabadiliko ya tabianchi Pangani, Tanga ni dhahiri- Afisa Mifugo

Kadri siku zinavyosonga hivi sasa, shughuli za binadamu zinavyoshamiri, vivyo hivyo mabadiliko ya tabianchi ambayo nayo yanazidi kuwa dhahiri miongoni mwa wakazi wa maeneo mbalimbali. Kila sekta imeguswa. Hali inakuwa ni changamoto zaidi kwa wakazi walio karibu na fukwe au wanaopakana na bahari. Mathalani nchini Tanzania kwa wakazi wa Pangani mkoani Tanga shughuli za kilimo,uvuvi na ufugaji zimeathirika na wanapaswa kuchukua hatua zaidi. Je madhara ni kwa kiasi gani?

Audio Duration
4'26"
UN News/ John Kibego

Mwanamke aliye na uleamvu wa kutoona aeleza madhila vitani, DRC – Sehemu ya 2

Karibu kwenye sehemu ya pili ya makala kuhusu madhila anayekumbana nayo mwanamke aliye na uleamvu wa kutoona kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kunusurika vita ingawa alimpoteza mumewe aliyekuwa akimkumbatia kabla ya vita vilivyomlazimisha kuvuka mpaka na kuingia Uganda.

Je, maisha yalikuwaje kipofu katika kambi ya wakimbizi? Je, ni msaada gani anaoutaka kusukuma maisha na ulemavu huo uuzeeni na ukimbizini.

Basi ungana na John Kibego aliyemtembelea katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali.

(Makala ya John Kibego)

Sauti
3'9"
© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Hatua zaidi zachukuliwa kukabiliana na COVID-19 nchini Kenya

Kufuatia raia wa Kenya kulalamikia hatua ya Rais wa nchi hiyo kutangaza zuio la kusafiri katika baadhi ya mikoa kwa mfano kuingia jijini Nairobi, Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna ameieleza idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa tangazo hilo la rais Uhuru Kenyatta halina nia ya kumuumiza mtu yeyote bali kuwakinga wananchi wote dhidi ya virusi vya corona, COVID-19. Hadi sasa Kenya imethibitisha kuwa na wagonjwa 172 baada ya watu wengine 14 kugunduliwa kuwa na virusi hatari vya corona kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Sauti
5'26"
UN News/ John Kibego

COVIDI-19 yazua changamoto za kupata huduma za afya Uganda

Kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona, COVID-19 kumezifanya nchi kukaza uzi zaidi katika hatua za kukabiliana na mlipuko huo ikiwemo vikwazo vya watu kutembea na hatua za kuwataka kusalia majumbani. Vikwazo hivi pamoja na kusaidia kudhibiti mlipuko wa COVID-19 lakini pia vimezua changamoto zingine. Mathalani nchini Uganda ambako kuna marufuku ya watu kutembea wagonjwa wengi wameanza kupata changamoto ya kufikia huduma za afya kutokana na maagizo mapya yanayolenga kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kama alivyobaini mwandishi wetu nchini humo John Kibego katika makala hii

Sauti
3'37"
World Bank / Sarah Farhat

COVID-19: Kufungwa kwa shule kunazua changamoto kwa wazazi na walezi kudhbiti watoto

Kutokana na kuenea kwa kasi kwa virusi vya corona, COVID-19 ambavyo vinashambulia mfumo wa upumuaji wa binadamu, serikali nyingiduniani zimelazimika kufunga shule ili kuwaepusha watoto na maambukizi ya ugonjwa huo hatari. Kufungwa kwa shule kunawafanya watoto kusalia katika makazi yao huku changamoto kwa wazazi au walezi ikiwa ni kuwadhibiti wasitoke kwenda kukutana na wenzao mtaani kushiriki michezo yao ya kawaida.

Sauti
3'48"
UN Photo/Loey Felipe

Kampuni ya ZuRi Africa yajitosa kusaidia harakati dhidi ya COVID-19 Tanzania

Kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona, COVID-19, maeneo mbalimbali duniani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukisihi wadau kujitokeza kuunga mkono hatua za kimataifa na kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo visivyo na tiba wala chanjo. Wito huo umeitikiwa vyema nchini Tanzania ambako kampuni binafsi zimejitokeza kuunga mkono serikali na miongoni mwao ni ile ya ZuRi Africa. Je wao wamefanya nini?

Sauti
4'15"
WFP

Wakimbizi wakosa mgao wa chakula kufuatia marufuku ya usafiri wa umma, Uganda

Nchini Uganda kama ilivyo katika maeneo mengine duniani imeimarisha hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Corona au COVID-19 kutokana na  ongezeko la wagonjwa.

Hatua hizo zikiwa ni pamoja na kufunga tasisi zote za elimu na kupiga marufuku usafiri wa umaa vimekuwa na madhara makubwa hususan kwa wakimbizi katika nchi hiyo yenye wakimbizi zaidi ya milioni 1.3.  

Sauti
3'45"
UN News/ Stella Vuzo

Elimu kwa jamii kuhusu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona Tanzania

Wakati ulimwengu unaendelea na mapambano dhidi ya virusi vya corona, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaeleza wasiwasi wake kuhusu elimu ya watoto kutokana na ulazima wa kufungwa kwas hule katika mataifa takribani 120 hivi sasa duniani kote. Shirika hilo linasema zaidi ya nusu ya wanafunzi wote ulimwenguni wameathiriwa na hatua ya kufungwa kwa shule ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Sauti
4'5"