Wanaoishi katika makazi duni wanahitaji mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN-HABITAT
Mamilioni ya watu wanaoishi katika mitaa ya mabanda au makazi dunia kote duniani wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu, ukosefu wa maji safi na salama n ahata hali mbaya ya Maisha lakini kubwa zaidi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT ni kutokuwa na mnepo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Shirika hilo linasema vimbunga au mafuriko yanapozuka wao huwa wa kwanza kuathirika na hasara yake ni kubwa Zaidi kuliko wengine.