Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sehemu ya kunawa mikono hosptiali ya taifa Muhimbili, Tanzania yasaidia vita dhidi ya COVID-19

Sehemu ya kunawa mikono hosptiali ya taifa Muhimbili, Tanzania yasaidia vita dhidi ya COVID-19

Pakua

Wakati visa vya virusi vya corona vikiendelea kupanda kila uchao, mataifa yanahaha kuweka mikakati kuhakikisha kwamba yanalinda wananchi wake dhidi ya ugonjwa huo ambao umesambaa kote ulimwenguni huku ukisababisha vifo vya maelfu ya watu duniani kote.

Tanzania licha ya kwamba ina idadi ndogo ya wagonjwa waliothibitishwa lakini imeendelea kuweka mikakati mbali mbali kwa ajili ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo kupitia serikali na wadau wengine ikiwemo sekta binafsi. Moja ya miradi inayoendeshwa ni ule wa kuwekwa sehemu ya kunawa mikono kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili ambapo Stella Vuzo Afisa wa Habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania akiwa amevinjari kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili kushuhudia mradi wa Mo Dewj Foundation wa kuweka sehemu mahsusi ya kunawa mikono  kwa ajili ya wageni wanaofika pale hospitaliani, mgeni wa leo anaanza kwa kujitambulisha

Audio Credit
Loise Wairimu/ Stella Vuzo
Sauti
4'3"
Photo Credit
UN News/ UNIC Dar es Salaam