Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa jamii kuhusu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona Tanzania

Elimu kwa jamii kuhusu kuzuia kuenea kwa virusi vya corona Tanzania

Pakua

Wakati ulimwengu unaendelea na mapambano dhidi ya virusi vya corona, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaeleza wasiwasi wake kuhusu elimu ya watoto kutokana na ulazima wa kufungwa kwas hule katika mataifa takribani 120 hivi sasa duniani kote. Shirika hilo linasema zaidi ya nusu ya wanafunzi wote ulimwenguni wameathiriwa na hatua ya kufungwa kwa shule ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutokomeza ugonjwa huo.

Hata hivyo UNICEF inatoa mwongozo na ushauri kwa wazazi, walimu, wsimamizi na serikali kuhusu kuwafanya watoto waendelee kupata elimu hata wanapokuwa nyumbani na vilevile wakipata elimu kuhusu ugonjwa wa COVID-19 na hatua za kujikinga.

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine, wakati wizara ya elimu ikiweka mikakati bora ya watoto kusoma, wizara ya afya nayo inafanya juhudi kuhakikisha watoto wanatambua namna ya kujinda kama anavyoeleza Afisa habari wa wizara hiyo ya Afya ya Tanzania Bwana Gerald Chami katika makala hii iliyoandaliwa na John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kabambala/ Gerald Chami
Sauti
4'5"
Photo Credit
UN News/ Stella Vuzo