Mabadiliko ya tabianchi Pangani, Tanga ni dhahiri- Afisa Mifugo

Mabadiliko ya tabianchi Pangani, Tanga ni dhahiri- Afisa Mifugo

Pakua

Kadri siku zinavyosonga hivi sasa, shughuli za binadamu zinavyoshamiri, vivyo hivyo mabadiliko ya tabianchi ambayo nayo yanazidi kuwa dhahiri miongoni mwa wakazi wa maeneo mbalimbali. Kila sekta imeguswa. Hali inakuwa ni changamoto zaidi kwa wakazi walio karibu na fukwe au wanaopakana na bahari. Mathalani nchini Tanzania kwa wakazi wa Pangani mkoani Tanga shughuli za kilimo,uvuvi na ufugaji zimeathirika na wanapaswa kuchukua hatua zaidi. Je madhara ni kwa kiasi gani? Saa Zumo, wa radio washirika Pangani FM mkoani Tanga nchini Tanzania amezungumza na afisa kilimo ambaye katika makala hii anaanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Loise Wairimu/ Saa Zumo
Audio Duration
4'26"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi