Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampuni ya ZuRi Africa yajitosa kusaidia harakati dhidi ya COVID-19 Tanzania

Kampuni ya ZuRi Africa yajitosa kusaidia harakati dhidi ya COVID-19 Tanzania

Pakua

Kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya ugonjwa wa Corona, COVID-19, maeneo mbalimbali duniani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukisihi wadau kujitokeza kuunga mkono hatua za kimataifa na kitaifa za kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo visivyo na tiba wala chanjo. Wito huo umeitikiwa vyema nchini Tanzania ambako kampuni binafsi zimejitokeza kuunga mkono serikali na miongoni mwao ni ile ya ZuRi Africa. Je wao wamefanya nini? Ahimidiwe Olotu, mwanahabari anayefanya mafunzo kwa vitendo kwenye kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC, jijini Dar es salaam, nchini Tanzania amezungumza na mkurugenzi wa kampuni hiyo Jestina George-Meru. Ungana nao kwenye makala hii.

Audio Credit
Loise Wairimu/ Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
4'15"
Photo Credit
UN Photo/Loey Felipe