Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya virusi vya Corona, COVIDI 19 ni jukumu la kila mtu:UN

Vita dhidi ya virusi vya Corona, COVIDI 19 ni jukumu la kila mtu:UN

Pakua

Kufuatia kusambaa kwa mlipuko wa virusi vya Corona COVID-19 sehemu mbalimbali duniani Umoja wa Mataifa na mashirika yake umekuwa ukihimiza kila mtu kuchukua hatua ili kuhakikisha ugonjwa huu hatari ambao umeshakatili maisha ya maelfu ya watu na kuathiri malaki ya wengine hausambai zaidi.

Kila nchi zimejiwekea mikakati ambayo pia inashirikisha wadau mbalimbali kuanzia ngazi ya jamii . Katika baadhi ya nchi kwa kiasi kikubwa wito unaitikiwa na miongoni mwa wanaoitikia wito huo ni madereva wa usafiri wa abiria wa pikipiki jijini Dar es salaam nchini Tanzania maarufu kama bodaboda ambao sasa wamechukua jukumu la kusambaza ndoo na sabuni kwa ajili ya wateja wao na wasafiri wengine kunawa mikono kabla ya kupanda kwenye vyombo hivyo vya usafiri ili kujikinga na ugonjwa huu wa Corona. Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC Dar es salaam amewatembelea madereva hao ambao wengi ni vijana kazini kwao na kuzungumza nao

Audio Credit
Loise Wairimu/ Stella Vuzo
Audio Duration
4'6"
Photo Credit
UN/Isaac Billy