Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wakimbizi wahusishwa katika kupambana na COVID-19 Uganda

Watoto wakimbizi wahusishwa katika kupambana na COVID-19 Uganda

Pakua

Mlipuko wa COVID-19 duniani umetia mashakani karibu malengo yote ya Maendeleo endelevu au SDGs baada ya kukwamisha elimu, usafiri na uchumi miongoni mwa mengine. Hali imekuwa mbaya zaidi miongoni mwa wakimbizi kutokana na changamoto za uhaba wa rasilimali ambazo kawaida huwakumba hasa idadi yao inapoongezeka  bila kutarajiwa. Hata hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameanzisha ushirikishwaji wa watoto wakimbizi katika juhudi za kupambana na COVID-19 wakati huu ambapo takribani wakimbizi mia moja wameambukizwa. Je, wanashirikishwa vipi? Ungana na John Kibego katika makala ifuatayo.

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
3'24"
Photo Credit
© UNHCR/Rocco Nuri