Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaowafanyia ukatili watoto ni muhimu waadhibiwe kwa uwazi-Morogoro

Wanaowafanyia ukatili watoto ni muhimu waadhibiwe kwa uwazi-Morogoro

Pakua

Wadau wa haki za watoto wanaopambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Morogoro Tanzania kwa kushirikiana na serikali na wadau, wamefanya mkutano kujadili namna ya kukomesha matendo hayo katika jamii. 

Taarifa ya ofisi ya Afisa ustawi wa jamii ngazi ya mkoa kuhusu matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya mama na mtoto mkoa wa Morogoro kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu inasema jumla ya matukio 2848 ya ukatili yaliripotiwa, kati yake matukio 1561 walifanyiwa watu wazima na matukio ya ukatili 1287 walifanyiwa watoto. John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro anaeleza mikakati waliyojiwekea wadau hao kuanzia kwenye ngazi za jamii hadi mkoa. 

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kabambala
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
UN Women