Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msitu wa Bugoma ni uhai kwa maisha yetu-Uganda

Msitu wa Bugoma ni uhai kwa maisha yetu-Uganda

Pakua

Misitu ya asili kote duniani, kwa miaka mingi imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Mathalani nchini Uganda, msitu wa Bugoma si tu unatunza historia ya asili ya watu wa eneo hilo, bali pia, wakazi wa eneo hilo wanasema vyanzo vingi vya maji ya mito ya eneo hilo ni katika mstu huo ambao pia unawapa dawa za asili za mitishamba zinazotumika katika tiba ya asili ya kiafrika. Katika makala ifuatayo, John Kibego, mwandishi wetu wa Uganda anapeperusha hewani maoni ya  wenyeji wa msitu wa Bugoma kuhusu tishio la kuchafuliwa kwa kiasi kukubwa cha msitu huo wa akiba.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
3'4"
Photo Credit
UNICEF/Tremeau