Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 imenirudisha nyumbani kijijini-Waweru

COVID-19 imenirudisha nyumbani kijijini-Waweru

Pakua

Tangu lizuke janga la corona duniani athari nyingi za karibu kila sekta zimeshuhudiwa. Vijana ambao idadi yao ndiyo kubwa kwa karibu kila nchini duniani nao wameathirika pakubwa. Wengi walilazimika kusitisha masomo kufuatia kufungwa shule na taasisi za elimu, wengine wakapoteza ajira na kubaki katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya maisha yao. Kijana Joseph Waweru alipoteza kibarua chake mjini Nairobi na pia mipango yake ya masomo katika chuo kikuu ikakwama ndipo akaamua kuhamia kwao alikozaliwa huko Kitale, magharibi mwa Kenya. Amezungumza na Jason Nyakundi kuhusu hali yake sasa na vijana wengine.

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
3'35"
Photo Credit
UN Kenya/Newton Kanhema