Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Ashley Gilbertson

Vita ya Urusi na Ukraine imevuruga uchumi wangu – Abeid Aboubakar wa Dodoma, Tanzania 

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hivi karibuni akizungumza na Baraza la Usalama alitaka hatua zichukuliwe kukomesha vita alipokuwa akizungumzia namna ambavyo ni vita ni chachu kubwa ya njaa duniani kote.  

Vita ya hivi karibuni ambayo imeongeza chumvi katika jeraha ni kutokana na uvamizi wa Urusi kwa Ukraine ambao pamoja na madhara mengine kwa ulimwengu, imeathiri uzalishaji na usambazaji wa mafuta ambayo ni bidhaa mtambuka kwa mambo mengi na inapoyumba inayumbisha karibu mihimili yote ya uchumi.  

Sauti
4'13"
UPU

Mitandao ya kijamii inatusaidia lakini habari za uongo nazo ni changamoto - Kambini Lusenda, DRC

Takribani miaka miwili iliyopita, Umoja wa Mataifa ulizindua mkakati wake na ukapewa jina "iliyothibitishwa" au “Verified initiative” ambao unataka watu kote duniani kutafakari kabla ya kusambaza taarifa au maaudhi kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ni moja ya njia inayotumiwa na jamii sio tu kwa mawasiliano kwa wapendwa wao bali pia kupata taarifa muhimu sehemu mbalimbali na za muhimu katika maisha ya kila siku.

Sauti
4'1"
United Nations

Unaelewa nini kuhusu “Usawa wa Kijinsia”? Baadhi ya vijana wanawake Tanzania wanaeleza

Umoja wa Mataifa unasema kuwa athari za kiuchumi na kijamii za janga la COVID-19 zimeathiri vibaya maendeleo ya hivi karibuni yaliyokuwa yamefikiwa katika usawa wa kijinsia. Unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana umeongezeka, ndoa za utotoni zinatarajiwa kuongezeka baada ya kuwa zimepungua katika miaka iliyopita. Gonjwa hilo limeonesha hitaji la hatua za haraka kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijinsia ambao bado umeenea ulimwenguni kote na umuhimu wa kurejea kwenye mbio za kufikia usawa wa kijinsia.

Sauti
4'49"
UN News/Thelma Mwadzaya

Chakula, elimu na maji ni mtihani mkubwa kwa waathirika wa ukame Turkana Kenya

Watu zaidi ya milioni 3 wameathirika vibaya na ukame nchini Kenya kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA huku eneo lililoathirika zaidi ni kaunti ya Turkana.

Maelfu ya watu wanahaha kupata mlo, Watoto imekuwa changamoto kwenda shule na maji ambayo ni uhai imekuwa bidhaa adimu kupatikana, sasa watu hao wanaililia jumuiya ya kimataifa kunyoosha mkono kunusuru uhai na maisha yao.

Sauti
5'37"
© UNOCHA

Mahitaji ya wakimbizi kambini Lusenda tunayatambua na tunayashughulikia

Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi warundi ya Lusenda katika mkoa wa kivu ya Kusini mashariki mwa DRC, wametoa malalamiko yao mbele ya mkuu wa ofisi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR katika ukanda wa kaskazini mashariki mwa DRC yenye makao yake mjini Goma. Jackie Keegan amepokea malalamiko hayo na kuahidi kuyafanyia kazi alipotembelea kambi hiyo. Mwandishi wetu nchini humo Byobe Malenga amefuatilia ziara hiyo na kutuandalia makala haya.

Sauti
3'53"
Warren Bright/UNFPA Tanzania

Ukatili wa kijinsia na uchumi vinachangia maambukizi ya VVU - Dreams Mbeya, Tanzania

Watekelezaji wa mradi wa Dreams  mkoani Mbeya nchini Tanzania, mradi unaowalenga vijana kati ya umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nne walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI, VVU na walio ambao tayari wana virusi vya UKIMWI, wanasema kuwa baada ya kugundua kuwa ukatili wa kijinsia na hali ya uchumi vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ueneaji wa mammbukizi ya VVU, ndipo waliamua kujikita na malengo kadhaa ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo  endelevu SDGs kama vile lengo namba 1 la kutokomeza umaskini, namba 3 kuhusu afya na ustawi bora na namba 5 la u

Sauti
4'33"
UN /Mark Garten

Tuwalete UN wale walio nje ili wapeleke ujumbe wetu; asema Bi. Mohammed akimkaribisha Burna Boy

Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy"  amefanya ziara kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Naibu Katibu Mkuu, Amina J. Mohammed. Bi. Mohammed ambaye ni raia wa Nigeria amesema wakati wa ziara hiyo kuwa Burna Boy ni raia mwenzangu kutoka Nigeria na katika taifa hilo wako wanamuziki wengi mashuhuri wanaotumia sauti zao kusongesha masuala ambayo pia Umoja wa Mataifa unapigia chepuo. Sasa ni bora kuwaleta walio nje ndani ya Umoja wa Mataifa ili wapeleke ujumbe wetu nje.

Sauti
3'15"
UN News/Video capture

Serikali ya Tanzania itakomboa watu wenye ulemavu kwa kuboresha mfumo wa ajira serikalini -  Shega Mboya

Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuboresha Sekretarieti ya mfumo wa uombaji ajira kwa njia ya mtandao maarufu kama Ajira Portal ili uweze kuwatambua watu wenye ulemavu na hivyo kumiza matakwa ya sera ya ajira ambayo ina kipengele mahususi kinacholenga kuwajumuisha watu wenye ulemavu.  Ushauri huo umetolewa na Shega Mboya wa Morogoro, Tanzania ambaye pamoja na kuwa na elimu ya juu ya digrii mbili, hajaweza kupata ajira ingawa anaamini pamoja na vigezo vingine ambavyo anaamini anavyo, laiti mfumo wa kidijitali ungeweza kutambua watu wenye ulemavu, ingekuwa rahisi kwake na kwa we

Sauti
2'40"
Acnur Brasil

Tunaishukuru UNHCR imetusaidia kubadilisha maisha – Watu wa asili ya Warao ukimbizini Brazil 

Kuelekea kuanza kwa Kikao cha 21 cha Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili ambalo litaanza Jumatatu wiki ijayo kwa kuwakutanisha katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jamii za watu wa asili, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeutumia mfano wa watu asili wa wa jamii ya Warao wa Venezuela walioko ukimbizini Brazil, kuonesha kuwa watu wa asili ni miongoni mwa makundi yanayoathiriwa zaidi na mizozo inapotokea katika jamii. Evarist Mapesa wa Redio washirika SAUT FM ya Mwanza Tanzania anaisoma taarifa hii.  

Sauti
2'49"