Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Patrick Brown

Watoto watumikishwao DRC wapaza sauti zao

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 wanatumikishwa kwenye kazi mbalimbali ikiwemo uchimbaji madini, ujenzi wa nyuma, na hata sokoni kwa lengo la kukidhi mahitaji ya familia za kutokana na hali ya umaskini. Mashirika ya kutetea hali ya watoto yanachukua hatua kusihi serikali kuhakikisha sheria za kumlinda mtoto zinazingatiwa ikiwemo kwenye machimbo ya madini. Lakini hali iko vipi , mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa huko DRC, Byobe Malenga amevinjari kwenye mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini ili kujionea hali halisi.
Sauti
3'20"
WHO/L. Pezzoli

Bunge lina nafasi kubwa ya kubadili mwelekeo wa afya ya jamii: Mbunge Nyongo

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limekuwa likizihimiza nchi zote duniani kuhakikisha zinafikia lengo la huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030 wakati huu ikiwa imesalia chini ya miaka 10 kufikia ukomo wa malengo hayo. Hata hivyo bado jamii nyingi hasa barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara lengo hilo ni mtihani na huenda nchi nyingi zisilifikie kwa asilimia 100 limesema shirika hilo. Je nini ni kikwazo kikubwa cha kufikia lengo hilo? Na serikali pamoja na mihimili yake likiwemo Bunge wanafaya nini kuhakikisha hatua zinapigwa?

Sauti
4'57"
UN News

Kongamano lafanyika Dodoma kujadili sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo Tanzania

Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya majanga yanayokumba dunia hivi sasa na kuathiri sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi. Nchini Tanzania kwa kutambua athari hizo hasi, kumefanyika kongamano la nane la mwaka 2022 la  sera kwa wadau wa sekta hizo, kongamano lilofanyika katika mji mkuu wa taifa hilo, Dodoma. 

Washiriki takribani 600 wametoka mikoa na pande mbalimbali ikiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Tanzania, serikali na sekta binafsi. 

Sauti
4'18"
UN Women/Ruth McDowall

Tanzania yazindua programu ya malezi, ustawi na makuzi ya watoto katika mikoa 10

Lishe duni ni moja ya changamoto mtambuka hususani katika ustawi na makuzi ya watoto. Kwa kulizingatia hilo na kwa kutambua kuwa kila nchi inapaswa kushiriki katika kuyasongesha malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endekevu, SDGs, Tanzania imezindua programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kumaliza changamoto ya lishe duni na changamoto nyingine dhidi ya watoto hususani walio chini ya umri wa miaka nane.

Sauti
3'37"
© UNDP/Amunga Eshuchi

Kila mtu ana jukumu la kulinda mazingira ya bahari

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani Umoja wa Mataifa unamchagiza kila mtu kuchukua hatua na kulinda mazingira ya bahari ambayo sio tu ni muajiri mkubwa wa sekta ya uvuvi duniani bali ni mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa duniani kote thamani ya soko la sekta ya bahari na rasilimali zake inakadiriwa kuwa ni dola trilioni 3 kwa mwaka au asilimia 5 ya pato la dunia ndio maana unaichagiza dunia kushikama kuchukua hatua kuilinda bahari kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Sauti
4'10"
FAO Tanzania

FAO na SIDO Tanzania yapatia mama lishe mafunzo ya usalama wa chakula

Tarehe 7 mwezi Juni kila mwaka ni siku ya usalama wa chakula duniani, ambapo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO, unaangalia ni kwa jinsi gani chakula kinaweza kuwa ni bora kwa mlaji bila kuathiri afya yake kuanzia shambani hadi mezani. Nchini Tanzania, FAO  imeshirikiana na shirika la viwanda vidogo nchini humo, SIDO na kupatia mafunzo mama na baba lishe katika majiji mawili ya mkoa wa Dodoma na DAr es salaam. Kulikoni?

Sauti
4'5"
Video ya IFAD

Sabrina Elba, Balozi mwema wa IFAD, aona jinsi miradi yanufaisha vijana kaunti ya Nyeri Kenya 

Mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea kukumba Dunia kila uchao hayajaacha wakulima salama. Nchini Kenya, wakulima vijana katika kaunti ya Nyeri, miaka miwili iliyopita walitegemea mto wa jirani na maji ya mvua kumwagilia mashamba yao ya mboga za majani. Hata hivyo ukame na mvua zisizotabirika vilivyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi vilikatisha wakulima tamaa.

Sauti
4'9"
UN/Ahimidiwe Olotu

Stadi za maisha ni muhimu hususan kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Nchini Tanzania Jumla ya Kaya 13,600 na vijana 2,700 wanatarajiwa kunufaika na tathmini ya upimaji stadi za maisha kwa kuangalia viwango vyao vya kujitambua, ushirikiano walionao kwao na kwa jamii, jinsi wanavyotatua matatizo pamoja na heshima binafsi jinsi wanavyojiheshimu wao, jamii na mali za wengine. Sifa zote hizo ni muhimu katika kusaidia wanajamii wa rika mbalimbali wanashiriki katika kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. 

Sauti
4'7"
MINUSMA/Harandane Dicko

Tunashirikisha makundi mengi ili kuhakikisha utulivu Mali - MINUSMA 

Kuwalinda raia dhidi ya vitisho vya unyanyasaji wa kimwili ni kiini au kitovu cha kazi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali. Kwa ujumla, misheni sita za kulinda amani kwa sasa zimeidhinishwa, chini ya mamlaka ya Ulinzi wa Raia, kutumia njia zinazofaa kuzuia au kukabiliana na vitisho vya unyanyasaji dhidi ya raia, ndani ya uwezo na maeneo ya operesheni, na bila kuathiri jukumu la serikali mwenyeji.

Sauti
3'11"