Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Vincent Tremeau

Wakati napigana msituni sikuweza kutunza familia, sasa mradi wa MONUSCO umeniinua- Aristote

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hali ngumu ya maisha inatumbukiza vijana katika mapigano ya msituni mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu. Kwa kubaini hilo, Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo  MONUSCO unatekeleza miradi kama ule wa kuvunja makundi yaliyojihami, kupokonya silaha wanamgambo na kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, mradi ambao unatamatishwa kwa kuwapatia wapiganaji hao wa zamani stadi za maisha ili wajipatie kipato.

Sauti
3'34"
UNICEF/Frank Dejongh

Wagonjwa wa TB fuateni ushauri wa daktari kama nilivyofanya mimi na nimepona - Oduor

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO linaeleza kuwa kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 pamoja na migogoro katika mataifa mbalimbali, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa kifua kikuu, TB ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mapambano ddhidi ya ugonjwa huu yalikuwa yanaendelea vizuri. Kifua Kikuu ni ugonjwa hatari unaohitaji muda mrefu kutibu na unaweza kuwa sugu kwa dawa, lakini vile vile una kinga ambayo ni chanjo.. Thomas Oduor ni mkazi wa Nairobi ambaye aligundulika kuuugua kifua kikuu sugu mwaka 2020 na kutibiwa kwa mwaka mmoja na nusu.
Sauti
3'51"
© UNICEF/Zahara Abdul

Mafuriko yavuruga ndoto za wanawake wa Ziwa Albert, Uganda

Mbali na janga la Janga la Corona au COVID-19 ambalo limeikumba dunia kwa zaidi ya miaka miwili, wananchi wa Uganda waishio karibu na Ziwa Albert kwa miaka hiyo miwili wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ziada ya mafuriko.

Wanawake wanachama wa kikundi cha Kaizo Women’s Group (KWG) wilayani Hoima ni moja wapo ya vikundi ambayo mipango yao ilikwamishwa na atahri za mafuriko na ambao sasa wanaomba msaada wa kifedha kutoka serikali katika juhudi zao za kujikwamua kutokana na uharibifu wa maji huku wakikabiliana na janga la COVID-19.

Sauti
3'32"
Unsplash/Redgirl Lee

Nukta Fakti na elimu kuhusu habari za uongo mtandaoni

Janga la Corona au COVID-19 lilipoibuka miaka miwili iliyopita halikuleta changamoto za afya pekee bali kiuchumu na masuala mengine ya kijamii kama hofu juu ya taarifa zihusianazo na janga hilo. Kwakuwa janga hilo lilikuwa jipya wananchi wengi walijikuta wakihamaki kutokana na kuenea kwa taarifa za uzushi zilizokuwa zikisambaa mitandaoni.

Sauti
4'8"