Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuwalete UN wale walio nje ili wapeleke ujumbe wetu; asema Bi. Mohammed akimkaribisha Burna Boy

Tuwalete UN wale walio nje ili wapeleke ujumbe wetu; asema Bi. Mohammed akimkaribisha Burna Boy

Pakua

Damini Ebunoluwa Ogulu al maaruf "Burna Boy"  amefanya ziara kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Naibu Katibu Mkuu, Amina J. Mohammed. Bi. Mohammed ambaye ni raia wa Nigeria amesema wakati wa ziara hiyo kuwa Burna Boy ni raia mwenzangu kutoka Nigeria na katika taifa hilo wako wanamuziki wengi mashuhuri wanaotumia sauti zao kusongesha masuala ambayo pia Umoja wa Mataifa unapigia chepuo. Sasa ni bora kuwaleta walio nje ndani ya Umoja wa Mataifa ili wapeleke ujumbe wetu nje. Hayo na mengine mengi yaliyojiri kwenye ziara hiyo utapata kwenye makala hii inayosimuliwa kwako na Assumpta Massoi.
 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'15"
Photo Credit
UN /Mark Garten