Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chakula, elimu na maji ni mtihani mkubwa kwa waathirika wa ukame Turkana Kenya

Chakula, elimu na maji ni mtihani mkubwa kwa waathirika wa ukame Turkana Kenya

Pakua

Watu zaidi ya milioni 3 wameathirika vibaya na ukame nchini Kenya kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA huku eneo lililoathirika zaidi ni kaunti ya Turkana.

Maelfu ya watu wanahaha kupata mlo, Watoto imekuwa changamoto kwenda shule na maji ambayo ni uhai imekuwa bidhaa adimu kupatikana, sasa watu hao wanaililia jumuiya ya kimataifa kunyoosha mkono kunusuru uhai na maisha yao.

Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya aliambatana na ziara ya mkuu wa OCHA Martin Griffith wiki hii kwenye kaunti hiyo kushuhudia hali halisi. Amezungumza na wakazi wa kaunti hiyo na kuandaa Makala hii.

Audio Credit
Thelma Mwadzaya
Audio Duration
5'37"
Photo Credit
UN News/Thelma Mwadzaya