Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unaelewa nini kuhusu “Usawa wa Kijinsia”? Baadhi ya vijana wanawake Tanzania wanaeleza

Unaelewa nini kuhusu “Usawa wa Kijinsia”? Baadhi ya vijana wanawake Tanzania wanaeleza

Pakua

Umoja wa Mataifa unasema kuwa athari za kiuchumi na kijamii za janga la COVID-19 zimeathiri vibaya maendeleo ya hivi karibuni yaliyokuwa yamefikiwa katika usawa wa kijinsia. Unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana umeongezeka, ndoa za utotoni zinatarajiwa kuongezeka baada ya kuwa zimepungua katika miaka iliyopita. Gonjwa hilo limeonesha hitaji la hatua za haraka kushughulikia kukosekana kwa usawa wa kijinsia ambao bado umeenea ulimwenguni kote na umuhimu wa kurejea kwenye mbio za kufikia usawa wa kijinsia. Lakini pamoja na juhudi hizo, je, watu wanaelewa ni nini maana ya usawa wa kijinsia? Ili kufahamu hilo, Philbert Alexander wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam, Tanzania, amezunumza na baadhi ya vijana wa kike katika mitaa ya jiji la biashara la nchi hiyo ya Afrika Mashariki, Dar es Salaam – Tanzania, ambayo uongozi za ngazi ya juu unashikiliwa na wanawake, mathalani Rais ambaye ni mwanamke, haikadhalika Spika wa Bunge la nchi hiyo.  

Audio Credit
Anold KayandaPhilbert Alexander
Audio Duration
4'49"
Photo Credit
United Nations