Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili wa kijinsia na uchumi vinachangia maambukizi ya VVU - Dreams Mbeya, Tanzania

Ukatili wa kijinsia na uchumi vinachangia maambukizi ya VVU - Dreams Mbeya, Tanzania

Pakua

Watekelezaji wa mradi wa Dreams  mkoani Mbeya nchini Tanzania, mradi unaowalenga vijana kati ya umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nne walio kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI, VVU na walio ambao tayari wana virusi vya UKIMWI, wanasema kuwa baada ya kugundua kuwa ukatili wa kijinsia na hali ya uchumi vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ueneaji wa mammbukizi ya VVU, ndipo waliamua kujikita na malengo kadhaa ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo  endelevu SDGs kama vile lengo namba 1 la kutokomeza umaskini, namba 3 kuhusu afya na ustawi bora na namba 5 la usawa wa kijinsia. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kabambala
Sauti
4'33"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania