Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

Sawa Wanawake Tanzania yakabidhi majengo mawili kwa serikali ya Tanzania kusaidia vita dhidi ya unyanyasaji wa watoto

Mwishoni mwa mwaka jana 2021, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lilisema mwaka huo ulikuwa wa machungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za watoto. Ingawa taarifa ya UNICEF ililenga katika mizozo ya muda mrefu na ile mipya ni wazi kuwa matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto na unyanyasaji dhidi yao, unaendelea kujidhihirisha katika maeneo mbalimbali duniani.

Sauti
4'2"
FAO Tanzania

Salvation Youth Group wa Kasulu Kigoma Tanzania waushukuru mradi wa KJP 

Mnamo mwaka 2017 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO, la Mpango wa Chakula Duniani WFP kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF pia Kituo cha Biashara cha kimataifa ITC, yaliamua kushirikiana kutekeleza mradi wa pamoja Mkoani Kigoma nchini Tanzania, KJP. Kupitia mradi huo unaowahusisha wanawake vijana na wanaume vijana kupitia kwenye vikundi vyao, kikundi cha Salvation Youth Group cha Kasulu Kigoma kimenufaika kwa kupewa mashine ya kutotolesha vifaranga vya kuku kupitia mradi huo.

Sauti
3'21"
UN SDGs

Vijana wanaweza kuchagiza SDGs ikiwa watapewa miongozo sahihi - Austine Oduor

Vijana wanaaminika kuwa kundi muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwani nguvu yao ikikutana na ubunifu, inaweza kufanikisha mambo mengi chanya kwa ulimwengu. Hata hivyo kundi hili likikosa miongozo na taarifa sahihi linaweza kuwa kikwazo cha maendeleo yanayotarajiwa. Ndio maana Austine Oduor wa nchini Kenya, aliamua kuanzisha miradi inayowasaidia vijana wa mtaa wa mabanda wa Mukuru kwa Njenga jijini Nairobi, Kenya ili waweze kuanzisha biashara zao na pia kuwapa ushauri kuhusu maisha bora kuwaepusha na uhalifu.

Sauti
3'17"
Patrick Zachmann/Magnum Photos for FAO

Tutumie elimu tulizonazo kwa vitendo kwa ajili ya ustawi wa jamii zetu – Dkt. Anthony Kiiza 

Ufugaji na kilimo ni moja ya mambo mtambuka ambayo yakifanikiwa yanachangia katika kufanikisha idadi kubwa ya malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs kati ya 17 ambayo yanalengwa kufikiwa ifikapo mwishoni mwa muongo huu, mwaka 2030.  

Mathalani lengo namba moja linazungumzia kutokomeza umaskini, namba mbili linaongelea kutokomeza njaa, namba tatu linaongelea afya bora, namba saba linazungumzia nishati bora na ambayo ni nafuu na lengo namba nane likizungumzia ukuaji wa uchumi. Malengo yote hayo yanaguswa moja kwa moja na kilimo.  

Sauti
3'48"
UN SDGs

Mkopo wa masharti nafuu kwa vijana Tanzania waleta kipato na kufungua ajira

Umoja wa Mataifa kupitia malengo yake ya maendeleo endelevu, SDGs ya mwaka 2015 unataka vijana wapatiwe kipaumbele katika kufanikisha malengo hayo ikiwemo namba moja la kutokomeza umaskini. Serikali zinachagizwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri na ndio maana nchini Tanzania mikopo isiyo na masharti kwa vijana imekuwa mkombozi kwa vijana mkoani Mbeya ambapo takribani vijana 10 mjini Tukuyu wilaya ya Rungwe wametumia mkopo waliopatiwa kununua mashine ya kisasa ya kufyatua matofali.

Sauti
3'24"
UN News/ John Kibego

Mchakato wa kuomba makazi katika nchi ya tatu ukirejea tutafurahi sana - Wakimbizi Kyangwali Uganda 

Mlipuko wa COVID-19 ulififiza mambo mengi ikiwemo mchakato wa wakimbizi kuomba hifadhi katika nchi ya tatu ambapo huwa na matarajio makubwa kama maisha kuwa bora na upatikanaji wa kazi. Wakimbizi huwa na matarajio mengi kuhusu kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ya ukimbizi kutokana na simulizi wanazosikia kutoka wenzao waliowatangulia kwenda ng’ambo. Hata hivyo ndoto zao ziikuwa zimetiwa mashakani na mlipuko wa COVID-19 ambapo mchakato wa kuomba hifadhi ulisitishwa.

Sauti
3'48"
UNDP Bangladesh/Fahad Kaizer

Nilishuhudia shida wanazopitia wenye ulemavu nikatafuta ufumbuzi

Umoja wa Mataifa unaamini uvumbuzi na ubunifu ni moja ya nyenzo za kufanikisha kuyatimiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Kwa wale ambao wamelielewa somo hilo, tayari wanafanyia kazi ushauri huo na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao. Mfano ni fundi Lincoln Wamae wa nchini Kenya.


Lincold Kenya anasema kutokana na alivyokuwa anaziona changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini mwake wanapokuwa wanaenda na kurejea kutoka katika shughuli zao za kila siku, kulimfanya kuanza kuwaza namna ya kubuni viti mwendo vya kuwasaidia.

Sauti
3'10"
Manglar Vivo Project, UNDP Cuba

Mikopo kwa Miradi ya Mazingira kuwa na riba rafiki : CRDB Bank Tanzania

Katika makala hii leo Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na Hailo Kabiki mtaalamu wa masuala ya mazingira wa benki ya CRDB nchini Tanzania ambayo mwezi Oktoba mwaka jana wa 2021ilipata dola milioni 100 kutoka mfuko wa mazingira duniani, GCF kufanikisha kilimo kinachojali mazingira.

Na Benki yenyewe ikatenga dola milioni 100 na hivyo kufanya iwe na dola milioni 200 za kukopesha watakaokidhi vigezo. Katika mahojiano haya Bwana Kabiki anaanza kwa kuelezea mradi huo na mchakato wake.

Sauti
3'43"
UN/ Jason Nyakundi

Mtaani hakuna kazi lakini kuna fursa tutumie tujikwamue – Dorcas 

Kijana Dorcas Mwachia anakaribia kuhitimu shahada ya uzamili huko nchini Kenya. Ingawa hivyo katika kuelekea kutamatisha safari yake amegundua kuwa hana uwezo kifedha wa kumalizia karo na njia pekee ni kubonga bongo ajikwamue yeye na nduguye. Pitapita ya mitaa ya Nairobi nchini Kenya ikamkutanisha na chupa zilizotumika ambazo kwake yeye akaona ni fursa, huku akisafisha mazingira na wakati huo huo anazitumia kutengeneza mapambo anayouza. Kipato mfukoni na mazingira yanakuwa safi na sasa ameweza kukamilisha karo ya Chuo Kikuu na mengine mengi.

Sauti
3'8"