Lengo la ujumuishi kwenye elimu na kutomwacha mtu yeyote nyuma ladhihirika Tanzania
Umoja wa Mataifa unatambua kuwa elimu ina uwezo mkubwa wa kumuinua mtu kiuchumi na kijamii, kwa maana ya kwamba ni silaha mujarabu ya kuondokana na umaskini. Kupitai malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lengo namba 4, Umoja wa Mataifa unataka elimu bora tena isiyomwacha mtu yeyote nyuma, kwa misingi ya rangi, eneo aliko au hali ya mwili wake. Tayari nchi na mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali yanafanikisha lengo hilo, mfano humo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa taifa hilo la Afrika.