Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi aliyerejea nyumbani Burundi kutoka Tanzania awaambia wenzake, "rejeeni nyumbani tujenge nchi yetu."

Mkimbizi aliyerejea nyumbani Burundi kutoka Tanzania awaambia wenzake, "rejeeni nyumbani tujenge nchi yetu."

Pakua

Akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini Burundi hivi karibuni, Naibu Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR Kelly Clements ameihi jamii ya kimataifa iongeze msaada kwa maeneo na jamii ambako wakimbizi wa Burundi wameamua kurejea nyumbani kwa hiari. 

Tangu mwaka 2017, zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Burundi wamerejea nyumbani kutoka nchi jirani kama vile Tanzania. 

Tayari UNHCR imekuwa ikisihi hatua zaidi zifanyike ili kuboresha mazingira kwenye maeneo ambako wakimbizi wanarejea Burundi ili urejeaji wao uwe endelevu. 

Ni katika ziara yake Bi.Clements ameshuhudia wakimbizi zaidi wakirejea kutoka Tanzania na kuzungumza nao, huku wale waliorejea siku nyingi nao wakitoa wito wao na wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC nao wakipaza sauti zao. Kwa kina fuatana na Assumpta Massoi kwenye Makala hii kutoka UNHCR. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'52"
Photo Credit
UNHCR Video