Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wenye ulemavu nao wanaweza kujipatia kipato

Wakulima wenye ulemavu nao wanaweza kujipatia kipato

Pakua

Inakadiriwa kuwa asilimia 20 ya watu maskini zaidi duniani wana aina fulani ya ulemavu. Watu wa vijijini wanaoishi na ulemavu wanakabiliwa na changamoto zaidi kuliko wenzao wa mijini ndio maana ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu ni lengo muhimu katika kutekeleza azma ya Mfuko wa umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD

IFAD tayari ina uzoefu katika kufanya kazi na watu wenye ulemavu. Katika miaka ya hivi karibuni, IFAD imekuwa ikiongeza juhudi zake za kuwajumuisha watu wote wenye ulemavu. 

Anold Kayanda anatupeleka nchini Kenya na Sierra Leone kuangazia miradi ya IFAD imekuwa ikiwasaidia wakulima wenye ulemavu kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine kama ugonjwa wa Covid-19.

Audio Credit
Selina Jerobon/Anold Kayanda
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
IFAD