Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia ya nyuklia yaleta matumaini kwa wakulima nchini Kenya

Teknolojia ya nyuklia yaleta matumaini kwa wakulima nchini Kenya

Pakua

Je ni kwa vipi teknolojia ya nyuklia inaweza kuleta tofauti katika uzalishaji wa chakula wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kugonga vichwa vya watu na kubisha hodi kila uchao? Baadhi ya watu wakisikia nyuklia kinachowajia kichwani ni mabomu ya nyuklia, lakini nchini Kenya, wanasayansi na wakulima wanaelezea kwa maneno yao wenyewe vile ambavyo sayansi ya nyuklia inasaidia kupambana na uhaba wa chakula na maji. Kuanzia uzalishaji wa mbegu mpya zinazohimili ukame hadi teknolojia za kutambua ni muda gani muafaka kumwagilia mazao. Utaalamu huu unafanyika kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya nyuklia, IAEA. Ungana basi na Leah Mushi kwenye Makala hii iliyoandaliwa na IAEA

Audio Credit
Flora Nducha/Leah Mushi
Sauti
4'43"
Photo Credit
IAEA Video