Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lengo la ujumuishi kwenye elimu na kutomwacha mtu yeyote nyuma ladhihirika Tanzania

Lengo la ujumuishi kwenye elimu na kutomwacha mtu yeyote nyuma ladhihirika Tanzania

Pakua

Umoja wa Mataifa unatambua kuwa elimu ina uwezo mkubwa wa kumuinua mtu kiuchumi na kijamii, kwa maana ya kwamba ni silaha mujarabu ya kuondokana na umaskini. Kupitai malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lengo namba 4, Umoja wa Mataifa unataka elimu bora tena isiyomwacha mtu yeyote nyuma, kwa misingi ya rangi, eneo aliko au hali ya mwili wake. Tayari nchi na mashirika ya kimataifa na yasiyo ya kiserikali yanafanikisha lengo hilo, mfano humo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa taifa hilo la Afrika. 

Shirika moja kutoka Korea Kusini  kwa ushirikiano na shirika la SAWA Tanzania wamefanikisha uwekaji wa vifaa kwenye maktaba ya mtandao au eLibray katika shule ya awali na msingi ambayo ni jumuishi na sasa walimu, wazazi na wanafunzi wameona nuru. Nini kimefanyika? Basi shuhuda wetu ni Hamad Rashid wa Radio WAshirika MVIWATA FM kutoka Morogoro nchini Tanzania. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Hamad Rashid
Sauti
5'3"
Photo Credit
Picha: UN News