Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© UNICEF/Sebastian Rich

WHO na serikali ya Kenya wasambaza chakula tiba kwa wenye utapiamlo

Shirika la Umoja wa mataifa la Afya duniani, WHO kwa ushirikiano na serikali ya Kenya wanasambaza msaada wa chakula tiba cha dharura mahsusi kwa watoto walio na utapia mlo sugu. Watoto hao wanatokea kaunti za Samburu, Turkana na Isiolo ambako ukame na njaa vimepiga kambi. Watoto takriban 10,000 watapata chakula hicho kilicho tayari kuliwa. Thelma Mwadzaya amefuatilia operesheni hiyo na kutuandalia Makala hii. 

Sauti
4'9"
Photo: UNICEF/Athanas Makundi

Mashirika ya UN yahaha kuwasaidia waathirika wa mizozo na ukame Baidoa Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO linasema idadi ya milipuko ya magonjwa iliyoripotiwa na pia dharura za kiafya zinazohusiana na tabianchi katika Ukanda wa Pembe ya Afrika zimefikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea karne hii, na hivyo kuzidisha janga la kiafya katika eneo ambalo watu milioni 47 tayari wanakabiliwa na njaa kali. Mfano wa hivi karibuni ni katika maeneo kadhaa ya Pembe ya Afrika kama Somalia.

Sauti
4'27"
Maktaba ya binafsi: Bruce na Elvis

Mchagua kazi si mfanyakazi, wasema vijana walioamua kujiajiri baada ya kutofanikiwa kuajiriwa Rwanda 

Changamoto ya ajira ni suala mtambuka duniani na waathirika wakubwa ni vijana ambao wengi wanahitimu masomo hadi ya vyuo kikuu lakini wanajikuta wakizunguka na vyeti kusaka ajira bila mafanikio. Kwa kutambua changamoto hiyo Umoja wa Mataifa umekuwa msitari wa mbele kuwachagiza vijana kuingia katika sekta ya ujasiriamali ambayo sio tu itawapunguzia changamoto ya ajira bali pia itawawezesha kujikimu kimaisha na kuzisaidia familia na jamii zao.

Sauti
4'6"
Picha: Video screenshot

UNCDF kugeuza maeneo ya Kigoma, Tanzania kuwa uchumi jumuishi wa kidijitali

Kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma (KJP), Shirika la Umoja wa Mataifa la mitaji UNCDF na wadau wake kadhaa wamewezesha uanzishaji wa vikundi vya kukopesha na kuweka akiba vya vijiji na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha wa wanakikundi ili kukabiliana na kikwazo cha kimfumo cha wanavijiji kukosa ushirikishwaji wa kifedha. Anold Kayanda anaeleza zaidi kupitia makala hii.

Sauti
3'57"
UN News

Iwe malori au baiskeli lazima vifaa vya shule vifikie watoto nchini Burundi

Tarehe 24  mwezi  huu wa Januari ni siku ya elimu duniani ikimulika mafanikio na changamoto za kufanikisha lengo namba 4 la kufanikisha elimu bora kwa kila mtu kokote aliko. Elimu bora ni pamoja na vifaa ikiwemo madaftari, vitabu na kalamu ambako kwa watoto wengine bado vinasalia kuwa anasa. Mathalani nchini Burundi ambako huko katika baadhi ya maeneo wazazi wanalazimika kufanya vibarua wao na watoto wao ili waweze kumudu madaftari ya shuleni.

Sauti
4'3"