Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo na utu wa kibinadamu vikikutana, wenyeji na wakimbizi wanastawi- UNHCR

Maendeleo na utu wa kibinadamu vikikutana, wenyeji na wakimbizi wanastawi- UNHCR

Pakua

Charlotte Fatuma na Neema Cenga ni wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na sasa wanaishi ukimbizini nchini Msumbiji katika jimbo la Nampula. Kwa sasa Charlotte ni mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, akiendesha biashara ya duka kwenye makazi ya wakimbizi ya Coranne huku Neema naye akijitahidi kulea na kusomesha watoto wake. Wanawake wote hawa wawili ni wanufaika wa mradi wa kusambaza umeme unaofanikishwa kwa ubia kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB na serikali ya Msumbiji Mradi unalenga kusambaza umeme kwa wakimbizi wa ndani walioko kambini na wakati huo huo kunufaisha pia wenyeji. Hapa ni sawa na kuua ndege wawili kwa jiwe moja! Kwa kina basi Assumpta Massoi anasimulia kwenye Makala hii iliyoandaliwa na UNHCR

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Audio Duration
4'28"
Photo Credit
UNHCR Video