Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima Morogoro nchini Tanzania wachukua hatua kulinda mbegu za asili

Wakulima Morogoro nchini Tanzania wachukua hatua kulinda mbegu za asili

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO linasema mbegu za mazao ni msingi mkuu wa uendelevu wa binadamu hasa katika kuhakikisha uhakika wa kupatikana kwa chakula. 

Duniani kote kuna watunzaji wa mbegu za asili za mazao mbalimbali ambazo kwa wakati mwingine huboreshwa kadri muda unavyokwenda. 

Katika maeneo mengi, wakulima wenyewe ndio wahifadhi wa mbegu hizi na licha ya mabadiliko ya tabianchi kuwa kikwazo kwa baadhi ya mbegu, wakulima hawajakata tamaa wanaendelea kutumia mbegu hizo kwa kutambua umuhimu wake wa kuhifadhi afya na rutuba ya udongo, licha ya kuchukua muda mrefu kutoa mazao tofauti na mbegu zilizoboreshwa. 

Nchini Tanzania, katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa taifa hilo, baadhi ya wakulima kwa kutambua ubora wa mbegu za asili wamechukua hatua kuzitunza na wakati huo kuhifadhi mazingira ili yaweze kutoa mazao bora. Je wanafanya nini? Hamad Rashid, wa redio washirika MVIWATA mkoani humo amezungumza na baadhi ya wakulima na wataalamu na kuandaa Makala ifuatayo. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Hamad Rashid
Audio Duration
5'14"
Photo Credit
Picha: UM