Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Girl Shine ya UN Women imenijengea kujiamini na sasa nasaidia familia yangu- Rachael

Girl Shine ya UN Women imenijengea kujiamini na sasa nasaidia familia yangu- Rachael

Pakua

Mizozo na umaskini wa kupindukia kwenye mazingira ya uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu huwaweka wasichana katika hatari kubwa ya kukumbwa na ukatili na kunyanyaswa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN WOMEN kwa kutambua hilo linatekeleza miradi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini Kenya ili kuwajengea uwezo wasichana barubaru ili hatimaye waweza kuandaa mustakabali bora wa maisha yao. Girls Shine ni moja ya miradi hiyo kupitia mradi mkubwa wa LEAP unaoungwa mkono na serikali ya Japan tangu mwaka 2018. Wasichana wakimbizi na wenyeji wananufaika na mradi huu na sasa wanapaza sauti kama katika Makala hii iliyoandaliwa na UN Women barani Afrika na kusimuliwa na Thelma Mwadzaya.

Audio Credit
Leah Mushi/ Thelma Mwadzaya
Audio Duration
3'13"
Photo Credit
UN Women