Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za Hope for Girls and Women in Tanzania kupigania haki za kijamii nchini Tanzania

Harakati za Hope for Girls and Women in Tanzania kupigania haki za kijamii nchini Tanzania

Pakua

Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa Haki ya kijamii inafanya jamii na uchumi wa jamii hizo kufanya kazi vizuri na kupunguza umaskini, ukosefu wa usawa na mivutano ya kijamii. Haki ya Kijamii ina jukumu muhimu katika kufikia njia shirikishi zaidi na endelevu za maendeleo ya kijamii na kiuchumi na ni muhimu kwa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ndio maana Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau na kila mtu kushiriki katika kuhakikisha haki za kijamii zinalindwa. Na kwa msingi huo tunaangazia shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, shirika ambalo lina makao makuu yake Mugumu, wilayani Serengeneti, mkoani Mara kaskazini magharibi mwa Tanzania. Robi Samuel ni Mkurugenzi wa shirika hilo anaeleza shughuli wanazozifanya katika kupigania haki za kijamii hususani kwa wanawake na wasichana.   

Audio Credit
Selina Jerobon/Robi Samuel
Audio Duration
3'50"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania