Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kulima tunalima lakini lishe bado ni changamoto tuchukue hatua- Mkulima Sarah

Kulima tunalima lakini lishe bado ni changamoto tuchukue hatua- Mkulima Sarah

Pakua

Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.

Mathalani nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO linafadhili mradi wa AgriConnect ambao pamoja na mambo mengine  unapatia wananchi, wake kwa waume stadi za mapishi sahihi ya jamii ya mikunde.

Hivi karibuni wakati wa siku ya mikunde duniani tarehe 10 mwezi huu wa Februari, FAO ilishindanisha washiriki wa mradi huo kufahamu ni nani bingwa zaidi wa mapishi ya mikunde kwa kutambua kuwa Tanzania ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa mikunde lakini ulaji wake bado unachangamoto. Sasa makala hii inamulika harakati za kuchagiza ulaji wa mikunde pamoja na majani yake na mwenyeji wetu ni John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro, Tanzania. Kwako John!

 

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kabambala
Audio Duration
4'55"
Photo Credit
UN News