Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Redio Ngoma ya Amani inachangia utunzaji wa amani hapa mashariki mwa DRC - Wasikilizaji

Redio Ngoma ya Amani inachangia utunzaji wa amani hapa mashariki mwa DRC - Wasikilizaji

Pakua

Katika Siku ya Redio Duniani mwaka huu wa 2023, UNESCO inaangazia redio huru kama nguzo ya kujenga amani na kuzuia migogoro. 

Redio inatazamwa kama chombo muhimu na sehemu muhimu ya kutunza amani. Redio hushughulikia visababishi na vichochezi vya migogoro, kabla hazijaweza kulipuka na kuwa vurugu. Inatoa mbinu mbadala ya kuzuia migogoro, au migongano ya maslahi, kuondoa kutoelewana, na kutambua masuala ya kutoaminiana. Hii inaweza kusaidia kukabiliana na chuki, hamu ya kulipiza kisasi, au nia ya kutumia silaha. 

Na sasa hii leo dunia ikiadhimisha siku hii ya Redio Duniani, mwandishi wetu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Byobe Malenga anaangazia Redio Ngoma ya Amani, kituo cha redio cha mjini Fizi jimboni Kivu Kusini kinachohamasisha amani hususani katika maeneo ya mashariki mwa DRC. 

Audio Credit
Selina Jerobon/Byobe Malenga
Audio Duration
4'25"
Photo Credit
UN News/Byobe Malenga