Penye nia pana njia :Mwanariadha Faith Kipyegon
Umoja wa Mataifa umekuwa ukichagiza wanawake kuingia katika fani mbalimbali ambazo ingawa zina idadi kadhaa ya wanawake lakini asilimia kubwa ni wanaume. Fani hizo ni pamoja na riadha.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukichagiza wanawake kuingia katika fani mbalimbali ambazo ingawa zina idadi kadhaa ya wanawake lakini asilimia kubwa ni wanaume. Fani hizo ni pamoja na riadha.
Umoja wa Mataifa unaamini michezo ni moja ya njia zinazoweza kuchangia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.
Katika kuchagiza amani na upendo miongoni mwa wakimbizi, kijana Fideli Karafuru Busimba mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anatumia kipaji chake cha usanii kusambaza ujumbe wa upendo na amani hasa wakati huu wa changamoto zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 akiwa ukimbizini nchini Uganda. Kijana huyu ambaye pia ana ujuzi wa uchoraji na useremala, anaomba kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ukimbizini akiamini kuwa itamsaidia kuepuka changamoto za kifedha zinazokwamisha ndoto zake katika maisha.
Tarehe 22 mwezi huu wa Septemba viongozi wa nchi na serikali wanaohudhuria mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa watashiriki mkutano wa ngazi ya juu wakimulika miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban la kupinga aina zote za ubaguzi ikiwemo rangi na makundi mbalimbali kama vile watu wenye ualbino. Nchini Tanzania hatua zimechukuliwa na sasa kuna mazingira rafiki kwa watu hao kama anavyosimulia Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, nchini humo alipotembelea mkoani Mwanza.
Kilimo hai kina mchango mkubwa katika kutimiza ajenda ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa SDG’’s hasa katika kulinda mazingira , kuhakikisha uhakika wa chakula na pia kutimiza moja ya vipengele vya lengo la afya bora. Kwa mujibu wa
Malengo ya maendeleo endelevu yanayofikia ukomo mwaka 2030, yanasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayeachwa nyuma licha ya hali yake ya kiuchumi au aliko na witikio wa kauli hiyo ni dhahiri miongoni mwa watu katika jamii. Wakfu wa Nivishe unaowasaidia vijana ni miongoni mwa walioitikia wito huo.
Je, wafahamu kwamba kuna fursa kati ya changamoto zilizosababishwa na mlipuko wa covid-19 duniani? Wakati baadhi ya watu wamevunjika moyo baada uchumi kudorora huku wengine wakikabiliwa na changamoto za malazi na upatikanaji wa chakula katika maeneo ya mijini, bado kuna matumaini ya kufanya makubwa zaidi ikiwemo uvumbuzi utakaosaidia hata baada ya corona.
Ukosefu wa ajira ni moja ya matatizo yanayoendelea kuukumba ulimwengu na hasa ikizingatiwa kuwa wahitimu katika ngazi mbalimbali ni wengi, lakini nafasi za ajira haziongezeki na pia kwa namna fulani kutokana na maendeleo ya teknolojia, nafasi hizo zinazidi kupungua.
Anita Soina wa nchini Kenya, msichana mwenye umri wa miaka 20 anasema anajiona ni kama alichelewa sana kujiunga katika harakati za kuyatetea mazingira ya ulimwengu. Anita Soina anaona kuna umuhimu mkubwa watoto kufahamu mapema katika umri mdogo kuhusu umuhimu wa mazingira bora ya ulimwengu na namna uharibifu wa mazingira unavyoweza kuhatarisha mstakabali wao. Kutokana na mtazamo huo, sasa Anita Soina yuko mstari wa mbele kuhakikisha kuwa vijana na hata watoto wamefunzwa umuhimu wa kutunza mazingira.
Jamii ya wakimbizi ni miongoni mwa jamii zilizoatiriwa zaidi na mlipuko wa COVID-19 duniani kote kutokana na kuishi katiklka hali ya uhaba wa rasilimali ikiwemo chakula, dawa na malazi.
Kwa mantiki hiyo wadau mbalimbali wanoshirikiana na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na ofisi ya waziri mkuu wanashirikisha wakimbizi na viongozi wao kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo hasa katika ukatili wa kijinsia na huduma za afya ya uzazi.
Je, wanafanyaje?