Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na kusoma, ulimwengu wa sasa unahitaji uwe mbunifu - Underay Mtaki

Pamoja na kusoma, ulimwengu wa sasa unahitaji uwe mbunifu - Underay Mtaki

Pakua

Ukosefu wa ajira ni moja ya matatizo yanayoendelea kuukumba ulimwengu na hasa ikizingatiwa kuwa wahitimu katika ngazi mbalimbali ni wengi, lakini nafasi za ajira haziongezeki na pia kwa namna fulani kutokana na maendeleo ya teknolojia, nafasi hizo zinazidi kupungua. Nchini Tanzania, kijana Underay Mtaki ameligundua hilo na sasa anatumia ubunifu wake, ujuzi na elimu ya darasani kujiajiri kwenye sanaa ya uchoraji ili kuondokana na changamoto ya kukosa ajira na kujishughulisha na kazi zenye staha kama lisemavyo lengo namba nane katika malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Lucy Igogo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam Tanzania amezungumza na kijana huyo na kuandaa makala ifuatayo.

Audio Credit
John Kibego/ Lucy Igogo/ Underay Mtaki
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UN Nairobi/Duncan Moore