Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakfu wa Nivishe mkombozi kwa vijana wenye matatizo ya afya ya akili Kibera Kenya

Wakfu wa Nivishe mkombozi kwa vijana wenye matatizo ya afya ya akili Kibera Kenya

Pakua

Malengo ya maendeleo endelevu yanayofikia ukomo mwaka 2030, yanasisitiza umuhimu wa kuhakikisha kwamba hakuna mtu atakayeachwa nyuma licha ya hali yake ya kiuchumi au aliko na witikio wa kauli hiyo ni dhahiri miongoni mwa watu katika jamii. Wakfu wa Nivishe unaowasaidia vijana ni miongoni mwa walioitikia wito huo. Mwandishi wetu wa Nairobi Kenya Jason Nyakundi kutaka kujua mengi kuhusu wanachokifanya amezungumza na Amisa Rashid Ahmed, mshauri kweye wakfu huo wa Nivishe unaotoa huduma katika mtaa wa mabanda wa Kibera mjini Nairobi ukijikita katika kuwahudumia vijana wanaosumbuliwa na matatizo ya akili ambayo mara nyingi huletwa na changamoto za maisha ambazo vijana hawa hupitia kama vile umaskini na matumizi ya mihadarati.

Audio Credit
Grace Kaneiya/Jason Nyakundi/ Amisa Rashid Ahmed
Sauti
3'29"
Photo Credit
Picha ya maktaba ya UM