Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

"Ningekuwa mbali katika muziki isingekuwa vita" – Mkimbizi nchini Uganda

"Ningekuwa mbali katika muziki isingekuwa vita" – Mkimbizi nchini Uganda

Pakua

Katika kuchagiza amani na upendo miongoni mwa wakimbizi, kijana Fideli Karafuru Busimba mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anatumia kipaji chake cha usanii kusambaza ujumbe wa upendo na amani hasa wakati huu wa changamoto zinazotokana na mlipuko wa COVID-19 akiwa ukimbizini nchini Uganda. Kijana huyu ambaye pia ana ujuzi wa uchoraji na useremala, anaomba kupatiwa hifadhi katika nchi ya pili ukimbizini akiamini kuwa itamsaidia kuepuka changamoto za kifedha zinazokwamisha ndoto zake katika maisha. Ungana naye katika makala ifuatayo akizungumza na mwanndishi wetu wa Uganda, John Kibego.
 

Audio Credit
Leah Mushi / John Kibego
Audio Duration
3'42"
Photo Credit
UN News/ John Kibego