Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Penye nia pana njia :Mwanariadha Faith Kipyegon 

Penye nia pana njia :Mwanariadha Faith Kipyegon 

Pakua

Umoja wa Mataifa umekuwa ukichagiza wanawake kuingia katika fani mbalimbali ambazo ingawa zina idadi kadhaa ya wanawake lakini asilimia kubwa ni wanaume. Fani hizo ni pamoja na riadha. Wanawake wanaoshiriki fani hiyo wanasema kuna changamoto zake hasa pale unapokuwa na majukumu mengine ya familia , lakini wanaamini kwamba kazi yoyote ukiweka nia pana njia.Na mmoja wa wanawake hao ni mwanariadha kutoka Kenya Faith Kipyegon ambaye anawapa ushauri wasichana na wanawake wengine kutoacha ndoto zao za maisha ikiwemo kupata familia wakati wakiendelea na mambo mengine kwani yeye ameweza na hivi karibuni  ameweka rekodi mpya ya dunia ya kukimbia kwa  dakika 3 sekunde 53 na nukta 11 katika mashindano ya Olimpiki  yaliyofanyika mwaka huu Tokyo Japan . Amezungumza na mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi 

Audio Credit
Flora Nducha/Jason Nyakundi
Audio Duration
2'25"
Photo Credit
UNMISS