Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi wenye ualbino waona nuru, ni matunda ya azimio la Durban

Wanafunzi wenye ualbino waona nuru, ni matunda ya azimio la Durban

Pakua

Tarehe 22 mwezi huu wa Septemba viongozi wa nchi na serikali wanaohudhuria mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa watashiriki mkutano wa ngazi ya juu wakimulika miaka 20 tangu kupitishwa kwa azimio la Durban la kupinga aina zote za ubaguzi ikiwemo rangi na makundi mbalimbali kama vile watu wenye ualbino. Nchini Tanzania hatua zimechukuliwa na sasa kuna mazingira rafiki kwa watu hao kama anavyosimulia Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, nchini humo alipotembelea mkoani Mwanza.

Audio Credit
Stella vuzo
Audio Duration
4'1"
Photo Credit
UNICEF