Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wazungumzia changamoto za afya ya uzazi nchini Uganda

Wakimbizi wazungumzia changamoto za afya ya uzazi nchini Uganda

Pakua

Jamii ya wakimbizi ni miongoni mwa jamii zilizoatiriwa zaidi na mlipuko wa COVID-19 duniani kote kutokana na kuishi katiklka hali ya uhaba wa rasilimali ikiwemo chakula, dawa na malazi.

Kwa mantiki hiyo wadau mbalimbali wanoshirikiana na shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na ofisi ya waziri mkuu wanashirikisha wakimbizi na viongozi wao kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo hasa katika ukatili wa kijinsia na huduma za afya ya uzazi.

Je, wanafanyaje?

Mwandishi wetu w aUganda, John Kibego amehudhuria mjadala wa wakimbizi ulioandaliwa na shirika la Internews kwa kushirikiana na Spice FM katika makaazi ya wakimbizi ya Kyangwali.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
UN News/ John Kibego