Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Photo: IRIN/Mujahid Safodien

Taasisi ya PGWOCADE na harakati za kumkomboa msichana mkoani Rukwa Tanzania.

Mojawapo ya vikwazo vya harakati za kumwinua mwanamke kutoka katika hali duni iliyodumu tangu enzi na enzi mila na desturi za baadhi ya maeneo duniani ambayo wanajamii wamekwenda kwa kasi ndogo katika kuziacha mila hizo kandamizi na potofu. Licha ya ugumu huo, bado mazingira hayo hayapaswi kuwa kikwazo kwa wanarahakati ambao wanahaha kufikia  usawa wa kijinsia kwani mabadiliko ya mila na desturi hayawezi kuwa ya siku moja.

Audio Duration
4'27"
IOM/Amanda Nero

Wakazi wachukua hatua kulinda mto Nkumara Uganda

Maziwa, hifadhi za maji na mito vyote vina umuhimu mkubwa si tu kwa mazingira bali pia binadamu wanaozingira vyanzo hivyo vya maji. hata hivyo licha ya vyanzo hivi kuwa na umuhimu mkubwa kiuchumi, kimazingira na kiutamaduni bado vinakabiliwa na athari kutokana na shughuli za binadamu ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa vyanzo hivyo. Ulinzi kutokana na shuhguli hizo ni muhimu na ni kwa mantiki hiyo ambapo wakazi wa mto Nkumara nchini Uganda ambao wamechukua hatua kuandika katiba katika kuhakikisha ulinzi wa mto huo. Je kulikoni?

Sauti
3'57"
UN /MINUSCA

Kijana mkimbizi atumia radio chakavu kurusha matangazo huko kambini Kyangwali nchini Uganda

Leo Ijumaa katika makala kwa kina tuko nchini Uganda katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali, ambako John Safari, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ametumia ubunifu na ujuzi wa kukarabati redio na kuanzisha mtambo wa kurusha matangazo ya  redio yanachohabarisha jamii ya wakimbizi katika kambi ya Kyangwali nchini Uganda. Ungana na John Kibego katika mahojiano na mbunifu huyo.

Audio Duration
5'12"
Picha ya UN

PADI Ruvuma nchini Tanzania yasaidia utekelezaji wa lengo namba 10 la SDGs

Shirika la kiraia la PADI lenye lengo la kusaidia watu maskini na wenye ulemavu, limekuwa chachu ya maendeleo kwa wazee kwenye manispaa ya Songea mkoani Ruvuma nchini Tanzania. Shirika hilo limepanua mawanda yake ya usaidizi na kugusa maisha ya wazee kwa lengo la kusaidia waondokane na utegemezi na hivyo kuinua kipato chao sambamba na lengo namba 10 la malengo ya maendeleo endelevu la kupunguza pengo la kipato na hivyo kumkwamua mtu kiuchumi, Je PADI inafanya nini? John Kabambala wa radio washirika Kidstime FM amefunga safari hadi kwenye manispaa hiyo na kuzungumza na mmoja wanufaika bi.

Sauti
3'49"
Special Olympics

Sada Nahimana mfano dhahiri wa manufaa ya michezo

Michezo kwa amani na maendeleo ni kaulimbiu ambayo iko bayana katika malengo ya maendeleo endelevu ikimaanisha kuwa michezo inasaidia siyo tu kuongeza kipato bali pia kuleta utangamano kwa jamii na pia kuboresha maisha ya watu. Hii imedhihirika hasa kwa vijana hususan nchini Burundi.

Sauti
3'52"
Photo: UN Women/Ryan Brown

Wanawake wanaopigania haki wanasimamia kazi yao-Bi. Bisimba

“Wanawake labda kwa makuzi yao, wakifanya kitu wanafanya kwa kumaanisha,” hii ni sehemu ya maneno yake Helen Kijo Bisimba, mwanaharakati nguli wa kupigania haki za binadamu nchini Tanzania. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii Bi. Bisimba amesema wanawake ambao wanajihusisha na kupigania haki, ni kwa sababu wamepitia changamoto zitokanazo na ubinyaji wa haki na wanasimamia kazi yao. Basi ungana na Flora Nducha na Bi Kijo  kwa undani zaidi.

Sauti
3'38"
UN News/ Anton Uspensky

Athari za mabadiliko ya tabianchi hazina mipaka- mkaazi Bunyoro-Uganda

Lengo namba 13 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linachagiza mataifa kuchukua hatua za haraka ambazo zinaweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Lengo hilo limeorodhesha malengo madogo ambayo yatasaidia katika kufanikisha SDG 13 ifikapo mwaka 2030. Katika kupima utekelezaji wa lengo hilo, moja ya hatua ni kuimarisha uwezo wa kupanga na kusimamia mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika nchi maskini, visiwa vidogo na zile zinazoendelea, ikiwemo kwa kulenga wanawake,vijana na jamii mashinani na zilizotengwa.

Sauti
3'41"
ONU Info/Florence Westergard

Kutokata tamaa na UNHCR vimenifikisha hapa nilipo:Mkimbizi Bahige

Hadhi ya ukimbizi mara nyingi si hiyari bali changamoto na mazingira hulazimisha mamilioni ya watu kila uchao kufungasha virago na kukimbia patakapowasitiri. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wengi maisha yao huishia makambini, baadhi hukumbatiwa na jamii wakimbiliako, wengine huzogomwa na mitihani na wachache kama mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ya Rawhide jimboni Wyoming hapa Marekani, Bertine Bahige hupata fursa ya kupelekwa taifa la tatu kupitia mpango maalumu wa shirika la wakimbizi duniani UNHCR.

Sauti
4'39"
UNIDO

Kijana kutoka Tanzania atumia stadi alizozipata kuwezesha vijana wenzake

Lengo namba nane la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa linaangazia uchagizaji wa ukuaji uchumi endelevu na jumuishi na ajira yenye matokeo na kazi inayozingatia utu kwa wote.Katika kuangalia hatua zilizopigwa kufikia lengo hilo, takwimu zinaonyesha kuwa ukosefu wa ajira ulikuwa ni asilimia 5.7 mwaka 2016 huku idadi ya wanawake wasio na ajira ikiwa ni zaidi ya wanaume katika umri mbali mbali.

Sauti
4'47"