Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

PADI Ruvuma nchini Tanzania yasaidia utekelezaji wa lengo namba 10 la SDGs

PADI Ruvuma nchini Tanzania yasaidia utekelezaji wa lengo namba 10 la SDGs

Pakua

Shirika la kiraia la PADI lenye lengo la kusaidia watu maskini na wenye ulemavu, limekuwa chachu ya maendeleo kwa wazee kwenye manispaa ya Songea mkoani Ruvuma nchini Tanzania. Shirika hilo limepanua mawanda yake ya usaidizi na kugusa maisha ya wazee kwa lengo la kusaidia waondokane na utegemezi na hivyo kuinua kipato chao sambamba na lengo namba 10 la malengo ya maendeleo endelevu la kupunguza pengo la kipato na hivyo kumkwamua mtu kiuchumi, Je PADI inafanya nini? John Kabambala wa radio washirika Kidstime FM amefunga safari hadi kwenye manispaa hiyo na kuzungumza na mmoja wanufaika bi. Sophia Halfani, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee kwenye manispaa hiyo.

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/John Kabambala
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
Picha ya UN